Categories: Business

Kufungua Shauri na Uttetezi Mahakamani

16,000 TZS

Product description

Kama jina la kitabu lilivyo, mwandishi anaeleza kwa ufasaha kwa kutumia Kiswahili Sanifu, Utaratibu wa Kufungua Shauri linalohusu Mgogoro wa Ardhi katika Baraza la Ardhi la Kijiji, Baraza la Ardhi la Kata, Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya, Mahamak

Qty

Tab Article

Kama jina la kitabu lilivyo, mwandishi anaeleza kwa ufasaha kwa kutumia Kiswahili Sanifu, Utaratibu wa Kufungua Shauri linalohusu Mgogoro wa Ardhi katika Baraza la Ardhi la Kijiji, Baraza la Ardhi la Kata, Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya, Mahamaka Kuu na Mahakama ya Rufaa na jinsi ya kutoa ushahidi katika Mabaraza na Mahakama hizo, Wajibu na Haki za mdaawa akiwa Mahakamani.

Ikumbukwe kuwa, mahakama ziko pale kutoa haki, lakini, mdaawa asipofuata taratibu zinazotakiwa na sheria, anaweza kupoteza haki yake au haki yake kupewa mdaawa ambaye hakustahili kuipata.
Elimu hii ya Kufungua Shauri na Utetezi Mahakamani, mbali na kuhusu migogoro ya ardhi, inaweza pia kutumika kwa mashauri ya aina nyingine kwani kanuni ni zilezile.
Ieleweke kuwa, kutojua sheria, taratibu au kutokuwa na fedha zinazotakiwa kulipwa, hakutokupatia haki unayostahili. Kwa hakika, kutofuata taratibu na kutokuwa na fedha zinazotakiwa kulipwa kutakupotezea haki yako.

Kwa vile, mahali pekee pa mtu kupata haki yake ni mahakamani, kitabu hiki ni muhimu na cha lazima kwa kila mtu mzima, ikiwa ni pamoja na Viongozi wa Vitongoji, Mitaa, Vijiji, Kata, Tarafa, Wilaya na Mikoa, Wanasheria, Mahakimu na Mawakili.

0 reviews for Kufungua Shauri na Uttetezi Mahakamani

Add a review

Your Rating