Product description
Lengo kuu la mwanaume na mwanamke kufunga ndoa ni kuishi pamoja kwa furaha, kushirikiana, kujiletea maendeleo, kupata watoto na kuwalea pamoja hadi hapo kifo kitakapowatenganisha.
Hata hivyo, ndoa nyingi huzongwa na kutoelewana, kwa viwango tofauti,
..
read more
Lengo kuu la mwanaume na mwanamke kufunga ndoa ni kuishi pamoja kwa furaha, kushirikiana, kujiletea maendeleo, kupata watoto na kuwalea pamoja hadi hapo kifo kitakapowatenganisha.
Hata hivyo, ndoa nyingi huzongwa na kutoelewana, kwa viwango tofauti, baina yao. Kutoelewana huweza kukua hadi kuwa mgogoro. Migogoro ya ndoa ni jambo la kawaida kati ya wanandoa wengi.
Migogoro hiyo isiposuluhishwa matokeo yake ni ndoa kuvunjika, kitendo ambacho hakipendwi na jamii, na hakina faida kwa watoto wao, madhehebu ya dini, wazazi, jamaa na wategemezi wao. Athari za kuvunjika kwa ndoa ni nyingi na mbaya sana kwao, watoto wao na maendeleo yao.
Kwa vile, migogoro ya ndoa imekuwapo katika baadhi ya familia na itaendelea kuwapo, sheria imeanzisha Bodi za Usuluhishi wa Ndoa. Kazi za Bodi hizi ni mbili, yaani, kusuluhisha wanandoa na ikishindikana kutoa Hati kwa wanandoa hao ili waipeleke mahakamani kwa ajili ya kuvunja rasmi ndoa hiyo.
Kwa mujibu wa Sheria, chombo pekee chenye mamlaka ya kutamka kuwa ndoa imevunjika na kutoa Hati ya Talaka ni Mahakama. Mahakama nayo hutoa uamuzi huo baada ya kujiridhisha pasipo shaka, kuwa, ndoa hiyo imeishavunjika na haiwezi kurekebika tena.
Katika kitabu hiki, mwandishi (pichani), ambaye ni Wakili Mwandamizi, ameeleza vizuri masuala haya ya kutoelewana na migogoro baina ya wanandoa na namna ya kuisuluhisha. Aidha, kitabu kinaeleza njia za kufuata ili hatimaye mahakama itoe Hati ya Talaka.
Hiki ni kitabu muhimu na cha lazima kwa wanandoa wote na wale wanaokusudia kufunga ndoa. Kitabu hiki ni cha lazima pia, kwa Wajumbe wa Bodi za Usuluhishi wa Migogoro ya Ndoa, Mahakimu, Mawakili, Wanafunzi wa Sheria na jamii kwa ujumla.
read less