Tab Article
Kitabu hiki ni cha nne katika mfululizo wa vitabu vitano vya somo la Uraia na Maadili kuanzia Darasa la Tatu hadi la Saba. Kitabu hiki cha Mwanafunzi Darasa la Sita kimeandaliwa kulingana na Muhtasari na Mwongozo wa Mwalimu wa Kufundisha somo la Uraia na Maadili wa mwaka 2016, ambao umezingatia ujenzi wa umahiri kwa mwanafunzi. Maudhui yaliyomo katika kitabu hiki ni mwendelezo wa yale yaliyomo katika kitabu cha Uraia na Maadili Darasa la Tano. Maandalizi ya kitabu hiki, yamezingatia mwenendo na matarajio ya nchi yetu ya Tanzania katika kukujengauweze kuheshimu na kuithamini jamii yako, kuwa mwajibikaji na kuwa mstahimilivu. Kitabu hiki kina sura kumi na sita na kila sura imeundwa na vipengele kadhaa. Maudhui ya sura za kitabu hiki yamejengwa kwa njia ya matini, mazungumzo, visa, habari, michoro na picha. Kila sura ina mazoezi na kazi za kufanya mwanafunzi. Pia, ufafanuzi wa msamiati umetolewa mwishoni mwa kila sura ili kukusaidia kuelewa kwa urahisi zaidi.